mbeya city......MADE IN MBEYA……..
na abdul sudi.
na abdul sudi.
Timu ya soka
ya Mbeta City imefanikiwa kuendeleza wimbi la ushindi ugenini baada ya kuifunga
timu ya Mgambo shooting kwa goli moja kwa bila,kabla ya mchezo huo Mbeya City
iliwafunga Oljoro JKT ya Arusha
2-1,ikawafunga tena Rhino ya tabora kwa magoli 3-1 na leo tena imewafunga
Mgambo shooting goli moja bila.katika mchezo wa leo goli la Mbeya City
lilipatikana katika kipindi cha kwanza likifungwa na mshambuliaji wake hatari
Jeremiah Juma.kpindi cha pili Mgambo walijitahidi kulishambulia lango la Mbey a
City ili upta bao la kusawazisha lakini uhodari wa ngome ya City uliwanyima
nafasi ya kumfikia kipa wao.Akiongea baada ya mchezo kocha wa Mbeya City Juma
Mwambusi alisema anashukuru vijana wake wamepigana na kufanikiwa kupata point
zote tatu na sasa hvi anatazama mchezo ujao ambapo watacheza nyummbani na timu
ya JKT Ruvu.aliwashukuru mashabiki wa soka wa moa wa Mbeya waliosafiri kuifata
timu yao na kuwaahidi vijana wake watafanya kila wawezalo ili kuzidi
kufanikiwa.
Mbeya City
inatarajia kucheza na Ruvu JKT tarehe 19
mwezi huu jijini Mbeya na tarehe 26 mwezi huu watakua na kazi nzito ya
kukutana na ndugu zao wa TZ Prisons katika mechi inayotaraiwa kuvutia maelfu ya
wakaziwa jiji la Mbeya.

Mechi ya Tz. Prison na Mbeya city itakuwa na ushindani wa hali ya juu sana, hasa ukizingatia kwamba kiwango walichoonyesha Mbeya city ni cha kushangaza kutokana kwanza na ugeni wa timu yenyewe katika mashindano haya makubwa kabisa kwa ligi ya nyumbani, na kwa upande wa Tanznia Prison wameonyesha kiwango kizuri japo matokeo hayakuwa upande wao kwa kiasi fulani, naamini watapigana ili kujiweka katika mazingira mazuri katika msimamo wa ligi na pia kulinda heshima yao mbele ya timu hii ngeni lakini hatari sana katika ligi.
ReplyDelete