PETER MICHAEL
wa tz prisons
Katika mzunguko wa kwanza wa ligi
kuu ya Vodacom Tanzania bara, timu ya Tz Prisons haikua inaenda vizuri, ilikua
inasua sua mno, baadae wakaamua kubadili benchi la ufundi kwa kumuondoa kocha
Jumanne Chale na kumleta kocha mzoefu David Mwamaja. Hali hiyo kwa kiasi Fulani
imeleta mabadiliko kwani katika michezo mitano ya mzunguuko wa pili, imetoka
sare miwili na kushinda mitatu.
Juhudi kubwa zinafanywa na wachezaji na
benchi la ufundi kuhakikisha hawapotezi hata mchezo mmoja katika mzunguuko huu
wa lala salama.
Mmoja kati ya wachezaji wa timu hiyo
ambae ana kiu ya kuhakikisha hilo linafanikiwa ni Peter Michael, mshambuliaji
anayejua goli liko wapi, kwani katika msimu huu wa ligi hadi sasa ana magoli
nane na bado ana hamu ya kuongeza mengine.
![]() |
| PETER MICHAEL AKIZONGWA NA NYOSO |
“Ninajitahidi sana kushirikiana na
wenzangu ili tuweze kufanikisha hilo, kwani hata mashabiki wetu walikua
wametukatia tamaa kutokana na matokeo mabovu, siwalaumu hao mashabiki, hakuna
mtu anaependa timu inayofanya vibaya, na sisi ili kuwaita tena ni kujitahidi
kucheza vizuri na kupata ushindi, hapo nina uhakika mashabiki wetu watarudi na
kutupa sapoti ya nguvu” alisema Peter Michael.
![]() |
| PETER NA NYOSO |
“Tazama michezo yetu ya mzunguuko wa
pili, tumetoka sare na Coastal Union, tukawafunga Ruvu, kisha tukawafunga
Mtibwa kwao, baadae tukawafunga JKT na mwisho tumetoka sare ya ajabu na Azam
ambayo kama mwamuzi angechezesha kwa haki nina uhakika tungeshinda” aliongeza
Peter.
Peter Michael alizaliwa Dar na kusoma
shule ya msingi Juhudi na sekondari akasoma katika shule ya Makongo. Alikua
akicheza soka shuleni Makongo, na uswahilini akiichezea timu ya Mti Pesa Fc ya
Ukonga.
![]() |
| PETER MICHAEL(mwenye tshirt)AKIWA NA JIMY SHOJI. |
Mwaka 2011 akajiunga na Tz Prisons, na
katika msimu huu hadi sasa tayari ana magoli nane mfukoni, kishawafunga Yanga goli moja, mtibwa kawafunga
mara mbili,kisha akawafunga Mgambo, aliwafunga Azam jijini Mbeya,Ruvu shooting
na mawili akawafuga Ruvu Stars katika
ushindi wa magoli sita bila.
“Kinachonisaidia kufunga ni kutokana na
kucheza na ‘mafundi’ kama Jimmy Shoji ‘Gema’, Salum Kimenya,na Omega Seme pamoja na
wachezaji wengine tuliopo pamoja, maana tumezoeana sana hivyo inakua rahisi hata kutengeneza hizo nafasi”.
![]() |
| AKIWA NA WACHEZAJI WENZIE |
Akaongeza “sasa hivi timu yetu imeshika kasi, ingawa
hata mzunguuko wa kwnza tulikua tkicheza vizuri, lakini sasa hivi tunapata na
matokeo, hivyo tutajitahidi sana kuendelea ushinda ili tujiweke katika nafasi
nzuri” kisha akaongeza “Tunawaahidi mashabiki wetu mambo mazuri yanazidi
kuongezeka, kila ataekuja mbele yetu tunapigana nae tumshinde, waje kuona timu
yao inavyocheza mpira unaopita katika njia, kwa sasa hivi Tz Prison tuko vizuri
sana” alimalizia Peter Michael.





Wako vizuri
ReplyDeleteepukenimajungu mfanyevizuri zaidi
ReplyDelete