Simba yazinduka
Simba imezinduka baada ya kuifunga
Ruvu Shooting kwa magoli 3-2, katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara. Hadi mapumiko Simba walikua wakiongoza kwa magoli mawili yote
yakifungwa na Amis Tambwe.
Alifunga la kwanza katika dakika ya 25
baada ya kuuwahi mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo chipukizi wa Simba Said
Hamis Ndemla na kipa wa Ruvu alishindwa kuudaka, na alipoutema ndipo Tambwe
akauwahi na kufunga.
Na la pili alifunga katika dakika ya
35 kwa kuunganisha krosi nzuri iliyopigwa na beki wa kulia wa Simba, anaejituma
na kupanda mbele kila mara, Haruna
Shamte .
Ruvu Shooting walicheza vizuri
katikati lakini walikuwa wakishindwa kulifikia lango la Simba kutokana na ushirikiano mzuri uliokua
ukifanywa na walinzi wa Simba wakiongozwa na Josef Owino na Don Mosoti.
Hadi mapumziko matokeo yalikua ni
Simba mawili na Ruvu hawakupata kitu.
Kipindi cha pili Ruvu walikianza kwa kasi
na walikua wakionyesha dhahiri wanataka magoli, na walifanikiwa kupata goli la
kwanza kupita kwa Said Dilunga katika dakika ya 75 akiunganisha kona
iliyochongwa na Michael Pius.
Kabla hawajashangilia vizuri kiungo
mshambuliaji wa Simba Harun Chanongo alifunga bao la tatu katika dakika ya 78,
baada ya kupokea pasi toka kwa mkongwe Amri Kiemba.
Ruvu hawakukata tamaa na katika dakika
ya 82 Jerome Lambele aliyeingia badala ya Elias Maguri aliifungia timu yake bao
la pili kwa njia ya penati baada ya mchezaji mmoja wa Simba kuushika mpira
katika eneo la hatari.
msirudi nyuma sasa
ReplyDelete