yanga na ahly kucheza Alexandria
Mchezo
wa marudiano kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri umepangwa kufanyika katika
uwanja wa Harras el Hadoud uliopo Alexandria
Misri siku ya jumapili, badala ya jijini Cairo.
Waziri wa mambo ya ndani wa Misri
alipiga marufuku mchezo huo kufanyika jijini Cairo baada ya mashabiki wa Al
Ahly kufanya fujo na kujeruhi polisi 26 mara baada ya kwisha kwa mchezo kati ya Al Ahly na Saxien ya Tunisia. Mchezo huo umepangwa
kufanyika bila ya mashabiki.
Mkurugenzi wa Al Ahly, Sayed El Hafez
alipanga kuongea na uongozi wa Yanga kuhusiana
na mabadiliko hayo ya uwanja kwani kulikua na tetesi kwamba Yanga
wasingekubali kucheza nje ya Cairo.
Al Ahly walipoteza katika mchezo wa kwanza
uliochezwa jijini Dar kwa goli moja kwa bila

Mechi hii Yanga wananafasi kubwa ya kusonga mbele, wanachotakiwa ni kuwa makini tu. Uwezo wanao wanatakiwa kuweka nia pamoja na kuwa makini mchezoni
ReplyDelete