TZ PRISONS YA UKWELI
Ligi kuu ya soka Tanzania bara
imemalizika kwa Azam Fc kuchukua nafasi ya kwanza huku Yanga ikiwa ya pili na
timu ngeni katika ligi ya Mbeya City ikiwa nafasi ya tatu.
Haukua msimu mzuri sana kwa timu ya Tz
Prisons, kwani hadi dakika ya mwisho
ilikua ikipigania roho yake ili isishuke daraja. Ilianza ligi hiyo kwa kusua
sua lakini mzunguuko wa pili ilikua ni moto wa kuotea mbali.
Ilifanikiwa kubaki katika ligi hiyo baada ya kuifunga timu ya Ashanti
kwa goli moja kwa bila, katika mchezo uliochezwa uwanja wa jamhuri Morogoro. Mchezo huo ulihudhuriwa na mashabiki wengi kutoka jijini Mbeya waliosafiri ili kuipa sapoti timu yao.
![]() |
| mashabiki waliokuwa wakiishangilia Tz Prisons |
Goli hilo muhimu lilifungwa na mshambuliaji
wake hatari Peter Michael, ambae kwa msimu huu ameonyesha kua ni mmoja kati ya
washambuliaji wenye uhakika wa kufunga katika ligi hiyo.
Ukitazama kwa haraka haraka unaweza kusema
Tz Prisons hawakua na uwezo ndio maana wakawa katika nafasi hiyo, lakini si hivyo. Kwani ni moja
kati ya timu zilizoonyesha kiwango cha hali ya juu sana na cha ushindani. Ila kilikua
na matatizo madogo madogo ambayo walichelewa kuyapatia ufumbuzi.
![]() |
| mashabiki wakipongezana baada ya kunusurika kushuka darajaAdd caption |
Katika mchezo wa mwisho dhidi ya
Ashanti, walionyesha kiwango cha juu kiasi kila mtu aliyekuwepo uwanjani
alishangaa ni kwa nini wanapigania kushuka daraja badala ya kuwa katika nafasi
nne za juu.
“ Tatizo kubwa la kwanza lililowakuta
Tz Prisons ni kwamba walichelewa sana kubadilisha benchi la ufundi, kocha
Jumanne Chale hana uwezo wa kufundisha timu za madaraja ya juu, ndio maana hata
alipokwenda Rhino amewashusha daraja” aliongea Fernad Daudi Mwakilembe, mmoja wa mashabiki
waliokua wakiishangilia timu ya Prisons
uwanjani Jamhuri.
![]() |
| Ally Mlagha(kushoto) na Fernard Daudi Mwakilembe wakiwa na mlinzi wa Tz Prisons,Nurdin Chona. |
“hakua na mipango ya uhakika kuifanya timu
icheze vizuri , lakini toka alipokuja David Mwamwaja timu imebadilika na hata
uchezaji na ari kwa wachezaji imeongezeka sana” aliendelea kuongea.
Katika mchezo huo, goli pekee
lilipatikana kipindi cha pili na kuwafanya Ashanti wapate certificate ya
kucheza daraja la kwanza.
Nae Ally Mlagha aliyesafiri toka Mbeya kuipa nguvu timu hiyo alisema “unajua
Ashanti wametengenezewa sana mazingira ya kubaki ligi kuu. Lakini uwezo hawana,
ukitazama hata jinsi mchezo wao na Simba ulivyobadilishwa na kusogezwa mbele ili
tu wajue matokeo ya timu nyingine utaona kua walikua wakitaka Ashanti ibaki, na
hata uamuzi wa kusema mchezo huo uchezewe Morogoro, ilikua ni kutengeneza
mazingira tz prisons icheze bila mashabiki wake, kwa maana michezo yote miwili
dhidi ya Ashanti wamecheza ugenini”.
Prisons
waliwazidi kila idara Ashanti, na kama wangekua makini wangeweza kupata
magoli mengi zaidi. Ukuta wa timu hiyo uliokua ukiongozwa na Nurdin Chona, beki mwenye kujituma na kujua vilivyo kukabiliana na washambuliaji tofauti, ulikua imara na kuweza kuwadhibiti vilivyo washambuliaji hatari wa Ashanti
wakiongozwa na mshambuliaji mwenye kasi na akili Ally Kabunda.
![]() |
| kocha David Mwamwaja akingea na waandishi baada ya mchezo na Ashanti uwanja wa Jamhuri Morogoro. |
Baada ya mchezo huo kocha wa Tz Prisons, David Mwamwaja alisema amefurahishwa
na matokeo ya mchezo huo na kwa sasa wanaanza kujipanga ili msimu ujao timu iwe
na ubora zaidi ya ulioonekana mwaka huu. " ligi imekwisha, tunakwenda kutazama ni wapi tulikosea ili msimu ujao tujue jinsi ya kurekebisha na kuboresha zaidi, kikubwa ninapenda kuwapongeza sana wachezaji wangu, kwani kazi waliyofanya ni kubwa na ngumu sana" alimalizia kocha huyo aliyeisaidia sana Tz Prisons kubaki ligi kuu.





Pa 1 sana mbeya yetu
ReplyDelete