Monday, 13 October 2014

STARS YAAMKA

    Hatimaye timu ya Taifa ya Tanzania, iliwafurahisha mashabiki wake baada ya kuifunga timu ya Benin wa magoli 4 kwa 1.
    Nadir Haroub na Amri Kiemba walionyesha uzoefu wao baada ya kufunga goli la kwanza na la pili kabla ya Thomas Ulimwengu kuongeza la tatu na Juma Luizio kumalizia la nne.

Wednesday, 1 October 2014

MATOGORO, MCHEZAJI BORA WA MWEZI SEPTEMBER

matogoro,mchezaji bora wa mwezi September

Bodi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania, imemchagua Anton Matogoro waMbeya  City kuwa ni mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi September 2014. Amepata na zawadi ya pesa kiasi cha shilingi milioni moja.

Sunday, 28 September 2014

  Yanga    yawafunga   tz   prisons

     Yanga ilipata goli lake la kungoza la kiufundi llililofungwa na Coutinho katika dakika ya 34, baada ya Mrisho Ngasa kuchezewa vibaya ndipo mwamuzi akatoa adhabu hiyo.
      Kama hiyo haitoshi , dakika nne baadae Prisons walipata pigo jingine baada ya mshambuliaji wake wenye nguvu Jackob Mwakalobo kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano kwa mchezo mbaya.

Friday, 26 September 2014

SIMBA NA YANGA YAAHIRISHWA

SIMBA NA YANGA SASA OCTOBA  18

Shirikisho la soka Tanzania, TFF limesogeza mbele kwa wiki moja mchezo wa mahasimu wa jadi Tanzania, Yanga na Simba kwa wiki moja zaidi, na hivyo sasa utafanyika tarehe 18 octoba badala ya tarrehe 12 kama ilivyokua katika ratiba ya awali.. 

Monday, 22 September 2014

TZ PRISONS YAANZA VEMA
    Timu ya Tz Prisons, ilizima kelele za msemaji wa timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire, baada ya kuwafunga kwa mabao mawili kwa bila katika mchezo mzuri uliochezwa uwanja wa Mabatini Ruvu.

Saturday, 20 September 2014

KARIBUNI MBEYA CITY INAWASUBIRI

KARIBUNI
MBEYA CITY INAWASUBIRI
        Msimu mpya wa ligi umefika, Mbeya City inaanzia pale pale ilipoishia msimu uliokwisha.
Ilishika nafasi ya tatu, hakuna aliyetegemea hilo,  lakini liliwezekana,  na sasa hivi inatarajia kwenda juu zaidi. Ni kazi ngumu,  ukichukulia timu zote zitakua zinaipania Mbeya City, kwani wanajua wakifanya makosa muziki wa City ni mkubwa , wataadhirika.

Friday, 19 September 2014

Beno kakolanya
    TZ PRISONS ONE

Baada ya katikati ya msimu uliopita kuondokewa  na aliyekua kipa nambari moja wa Tz Prisons, Wilbert Mweta, mashabiki wa soka walitegemea timu hiyo itashuka daraja, kwani katika mzunguuko wa kwanza, ilikua ipo chini kabisa mwa msimamo wa ligi, hivyo kuondoka tena kwa kipa tegemeo kuliwapa wasiwasi wengi.